Waziri Mkuu agawa fimbo nyeupe kwa walemavu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akigawa fimbo nyeupe kwa watu wenye ulemavu wa kuona alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Fimbo Nyeupe na Miaka 60 ya Chama cha Wasioona Tanzania (TLB) ambayo kitaifa yamefanyika Mkoani Kilimanjaro jana Oktoba 25, 2024.