The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Aipongeza Simba na Namungo Bungeni -Video

0

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa leo Februari 13, 2021 ameipongeza Simba SC kwa kupata ushindi wa kwanza ugenini kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita jana usiku Kinshasa, DR Congo.

 

Simba ilishinda bao 1-0 dhidi ya AS Vita kwa mkwaju wa penalti uliowekwa wavuni na Chris Mugalu dakika ya 60 na kuipa uhakika wa alama tatu timu yake.

Majaliwa ameyasema hayo wakati akiahirisha vikao vya Bunge jijini Dodoma na wabunge wakilipuka kwa furaha kushangilia.

“Nawapongeza pia mabingwa wa soka Tanzania timu ya Simba SC kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi na jana kushinda mchezo wake wa kwanza ugenini dhidi ya AS Vita nchini DR Congo,” amesema Majaliwa

Waziri Mkuu pia amempongeza Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez kwa ubunifu wake wa kushirikisha Wizara ya Utalii na kuja na wazo la kuweka maneno ya ‘Visit Tanzania’ kwenye jezi za Simba ambazo zinazotumika katika hatua ya makundi kutokana na kanuni za CAF kutoruhusu kampuni za kubeti kutumika kwenye jezi za klabu.

 

Majaliwa amesema hatua hiyo ni ya uzalendo na kutangaza nchi kimataifa kwenye sekta ya utalii.

Wekundu wa Msimbazi tayari wameanza safari ya kurudi nchini wakitokea DR Congo.

Majaliwa pia amethibitisha kuwa Klabu ya Namungo inashikiliwa na Jeshi la Angola na kusema hizo ni sehemu ya siasa za mpira.

“Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania inaendelea kushughulikia jambo hilo, na naitakia kila la kheri Namungo katika mchezo wake wa kesho,” amesema Majaliwa

Leave A Reply