Waziri Mkuu Alivyoongoza Mbio Za Nmb Marathon

 

 

 

 

 

 

 

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa, Mwenyekiti wa Bodi ya NMB  Dk. Edwin Mhede (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa pili kulia) wakishiriki katika mbio za hisani za ‘NMB Marathon’ kwa ajili ya kukusanya kiasi cha fedha zitakazo tumika katika matibabu ya Fistula kwa kina mama wasio na uwezo, kwenye viwanja ya Leaders jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, wengine ni viongozi mbalimbali wa Serikali na taasisi za umma na binafsi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna wakijiandaa kukimbia mbio za hisani za ‘NMB Marathon’.

…Zaipuna (kulia) akimshukuru Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dk. Anna Makakala (wa kwanza kushoto) kwa kufika kushiriki mbio za hisani za ‘NMB Marathon’.

aadhi ya watoto na wazazi wao wakishiriki katika mbio za hisani za ‘NMB Marathon’ kwa ajili ya kukusanya kiasi cha fedha zitakazo tumika katika matibabu ya Fistula kwa kina mama wasio na uwezo.

Mmoja wa wakishiriki waliomaliza kukimbia mbio za hisani za ‘NMB Marathon  akipokea medali. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna akizungumza katika hafla ya mbio za hisani za ‘NMB Marathon’.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya NMB  Dk. Edwin Mhede (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla (kushoto) wakishiriki mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza mbio za hisani za ‘NMB Marathon’.

 

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa ameongoza kukimbia mbio za hisani za ‘NMB Marathon’ kwa ajili ya kukusanya kiasi cha fedha zitakazo tumika katika matibabu ya Fistula kwa kina mama wasio na uwezo, kwenye viwanja ya Leaders jijini Dar es Salaam.


Toa comment