Waziri Mkuu Ameongoza Kikao Cha Kamati Ya Kitaifa Ya Nishati Safi Ya Kupikia
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Februari 09, 2024 ameongoza kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Nishati safi ya kupikia, katika ukumbi wa Spika, bungeni jijini Dodoma.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.