Waziri Mkuu Aohofia Usalama wa Harry na Meghan, Malkia Afunguka

WAZIRI Mkuu wa Canada, Justin Trudeau amesema mazungumzo zaidi yanahitajika kuhusiana na gharama za usalama wa Mwanamfalme wa Uingereza, Harry na Meghan.

 

Trudeau ameyasema hayo baada ya Harry na mkewe kuamua kujiondoa kuwa washiriki wa muda wote katika utekelezaji wa majukumu ya Kifalme na badala yake wapate muda wa kuishi Uingereza na Amerika Kaskazini.

Malkia Elizabeth wa Uingereza amekubali kipindi cha mpito ambapo mwanamfalme Harry na mkewe Meghan watakuwa wakiishi Canada na Uingereza.

 

Amesema kwamba anaunga mkono hatua yao ya kuanza kujitegemea lakini ingekuwa vizuri zaidi iwapo wangeendelea kutekeleza majukumu yao ya kifalme kwa muda wa kudumu.

 

Katika taarifa baada ya mazungumzo yaliyofanyika Sandringham January 13, Malkia alisema anatarajia kwamba uamuzi wa mwisho utafanyika hivi karibuni.

#LIVE: RAIS MAGUFULI AKIWAAPISHA MABALOZI IKULU DAR


Loading...

Toa comment