The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Apokea Taarifa Ya Kamati Kuchunguza Moto Soko La Kariakoo

0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Julai 28, 2021 amepokea taarifa ya Kamati ya Uchunguzi wa tukio la moto uliyotokea katika Soko la Kimataifa la Kariakoo Julai 10, 2021 jijini Dar es salaam.

 

Mhe. Kassim Majaliwa amepokea taarifa hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa Kamati hayo, CP Liberati Sabas na kuahihidi kuwa serikali itayafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati hiyo.

 

Akizungumza baada ya kuipokea taarifa hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Mheshimiwa Majaliwa amewashukuru na amewapongeza wajumbe wa Tume hiyo kwa kazi nzuri iliyofanyika kwa weledi mkubwa.

Mheshimiwa Majaliwa amesema ataifikisha taarifa hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwani tukio hilo limewagusa watu ndani na nje ya nchi.

 

“Naahidi mbele yako Mwenyekiti kuwa Serikali nimeridhishwa na taarifa mliyo nikabidhi leo na mapendekezo yote mliyoyatoa yatazingatiwa.

 

Jumapili Julai 11, 2021 Mheshimiwa Majaliwa alipotembelea na kukagua hatua zinazoendelea kuchukuliwa kudhibiti moto katika soko la kimataifa la Kariakoo alitangaza kamati ambayo ilipewa kazi ya kuchunguza tukio hilo ili kubaini chanzo cha moto huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo CP Liberati Sabas amezishukuru Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na wajumbe wengine katika timu hiyo kwa ushirikiano walioutoa katika kufanikisha kazi hiyo “Mheshimiwa Waziri Mkuu kama haya tuliyoyabaini yakifanyiwa kazi matukio kama hayo hayatajirudia”

 

kamati hiyo aliyoiunda ambayo ilifanya kazi na kamati ya ulinzi na usalama iliyoanza kufanya kazi chini ya Mkuu wa Mkoa huo ilijumuisha Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu (Idara ya Maafa).

 

Wengine ni Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikujumuisha Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi, Zimamoto, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU). Pia Waziri Mkuu alizitaja Wakala wa Majengo, Shirika la Umeme (TANESCO), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Ofisi ya Taifa ya mashtaka, Wakala wa Umeme na Ufundi Tanzania (TEMESA)

Leave A Reply