The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu- Serikali Imeafiki Bunge Kutorushwa Live

5
1Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majiliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba matangazo ya bunge hayatarushwa yote live na Television ya Taifa kama serikali ilivyosema na tayari hatua hiyo imekwisha kuanza.
Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa Hai ambaye pia ni msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe aliyetaka kujua kwanini serikali imefanya maamuzi ya kuzuia wananchi wasione matangazo ya Bunge moja kwa moja.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema kwamba uamuzi wa kutoonyeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja uliombwa na chombo cha umma chenyewe kwamba hakina uwezo kujiendesha na uamuzi wao huo umeungwa mkono na serikali.

”Maamuzi ya chombo hiki yameungwa mkono na serikali na waziri Nape Nnauye amefanya kipindi maalum kuhusiana na jambo hilo na wananchi wameelewa vizuri na wameiunga mkono serikali kwamba matangazo yatarekodiwa na yatarushwa kama kipindi maalum usiku” Amesema Waziri Majaliwa.

Aidha chombo cha umma kitakuwa kinarusha matangazo ya moja kwa moja kwa muda wa maswali na majibu kwa serikali na baada ya hapo matangazo yatarekodiwa na kurushwa katika kipindi kiitwacho leo katika Bunge.

5 Comments
  1. Neema alex says

    Jamani eeeh fanyeni mnavyoweza mimi wala SIJALI, Kila mtu na Maisha yake.!!!!

    au wabunge wanaogopa wananchi watajua uwozo unaoendelea BABA WA TAIFA alikuwa anabana matumizi kini hii kali. sijui tunakwenda wapi sasa hata mtanzania kunyimwa haki zetu
    Tanzania niya amani urithi tulio achiwa na BABA WA TAIFA MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI.

  2. Neema alex says

    Jamani eeeh fanyeni mnavyoweza mimi wala SIJALI, Kila mtu na Maisha yake.!!!!

    au wabunge wanaogopa wananchi watajua uwozo unaoendelea BABA WA TAIFA alikuwa anabana matumizi lakini hii kali. sijui tunakwenda wapi sasa hata mtanzania kunyimwa haki zetu
    Tanzania niya amani urithi tulio achiwa na BABA WA TAIFA MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI.J amani Dunia wote tutapita, tuweke na utu

  3. Alex kihongole says

    Siungi mkono hoja ya serikali kutunyima uhuru wa kuwasikiliza wabunge tuliowachagua. Na tbc mmeshindwa kurusha matangazo ya direct basi mseme gharama tuwape wengine watangaze tuna wakongwe wa uwazi na ukweli ITV WAPENI KAZI KAMA MSHASHINDWA.kunani hapo nyuma ya pazia.NAKUMBUKA MWLM NYERERE ALISEMA WANANCHI WANA HAKI YA KUPATA HABARI KWA CHOMBO CHOCHOTE KILE KWA UWAZI NA UKWELI, SWALI JEEE? KWA NINI MNATUFICHA WANANCHI TUSIJUE UWEZO WA WABUNGE WETU TULOWACHAGUA???.NAMPA HONGERA SANA ZITTO KABWE NA UKAWA KWA KUONYESHA KUWAPENDA WANANCHI MASKIN KAMA MIMI MPENDA HAKI.LAKIN KUMBUKEN 2020 SIO MBALI WOTE WATAPIMA KIJAN NA UKAWA IPI BORA.TUJALI UTU SIO MABAVU.

  4. Alex kihongole says

    Nahisi kura yangu ishapotea.,

  5. azizasaid says

    naunga mkono na naomb waendelee kubana matumz ili kuepuk hasara za kipuuz

Leave A Reply