Waziri Mkuu Autubia Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA79) New York, Marekani
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia kwenye Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA79) New York nchini Marekani, Septemba 27, 2024. Mheshimiwa Majaliwa amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo.
Mheshimiwa Majaliwa amehutubia kwenye mkutano huo akiwa ni Waziri Mkuu wa Pili kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa. Septemba 27, 2010 aliyekuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda alihutubia baraza la 65 (UNGA65).