The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Azindua Bwalo Na Bweni Shule Ya Sekondari Kibasila

0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na viwango vya ujenzi wa bweni na bwalo kwenye shule ya Sekondari ya Kibasila iliyopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 1.13

Mhe. Majaliwa amesema hayo leo (Jumamosi, Oktoba 05, 2024) alipozundua jengo hilo ambapo amewataka wote watakaolitumia jengo hilo walinde miundombinu yake ili litumike kwa muda mrefu

Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. Samia amedhamiria kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu kote nchini.

Naye, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke amesema kuwa kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia wanafunzi wa kike 228 hasa wa kidato cha tano na sita kupata elimu bora katika mazingira ya karibu hivyo kusaidia kuongeza ufaulu.

Leave A Reply