The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Azindua Mitambo Ya Uchorongaji Na Vita Vya Utafiti Kwa Wachimbaji Wadogo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Juni 24, 2025 akizindua mitambo ya uchorongaji na vifaa vya utafiti kwa wachimbaji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Juni 24, 2025 amezindua mitambo ya uchorongaji na vifaa vya utafiti kwa wachimbaji wadogo kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akipokea maelezo kuhusu mitambo ya uchorongaji na vifaa vya kisasa vya utafiti vilivyolengwa kuwawezesha wachimbaji kuongeza tija na usalama katika shughuli za madini, wakati wa uzinduzi rasmi Juni 24, 2025.

Utoaji wa mitambo hiyo ni utekelezaji wa maono na msukumo wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwawezesha wachimbaji wadogo kutokana na mchango wao katika kuzalisha ajira, kuboresha kipato cha mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa Taifa.

HABARI KAMILI INAKUJA

Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.