The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Hariri Atangaza Kujiuzulu

BEIRUT: WAZIRI Mkuu wa LEBANON, Saad El-Din Rafik Al-Hariri ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wake huo kutokana na wananchi kuandamana kwa wiki mbili wakimtaka aachie madaraka.

 

Oktoba 17, mwaka huu, Serikali ilitangaza kuanza kukata kodi kwenye mazungumzo kupitia mtandadao wa WhatsApp.

 

Waziri Mkuu huyo amepata misukosuko ya kisiasa baada ya kudorora kwa uchumi wa Taifa hilo na kusababisha hali ngumu ya maisha.

 

Shule na Benki zimefungwa kwa siku 12 sasa kufuatia maandamano hayo, huku Waandamanaji wakifunga Barabara Kuu za Jiji la Beirut.

Comments are closed.