The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Afungua Maonesho Ya Nanenane Jijini Dodoma

0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 01, 2024 amefungua maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni.

Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhusu powertillers za Kampuni ya Uagizaji wa Matreka ya Agricom wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni, Agosti 01, 2024. Kampuni hiyo inatarajia kufungua kiwanda cha kuunganisha matrekta katika eneo la Viwanja vya Nanenane, Nzuguni.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia kichwa cha zao la alizeti wakati alipofungua maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni, Agosti 01, 2024. Kulia ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

Leave A Reply