WAZIRI MKUU MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA


WAZIRI mkuu wa zamani wa Algeria,  Ahmed Ouyahia,  alifikishwa mahakamani  jana (Jumapili) kuhusu tuhuma za ufisadi unaohusu shirika moja la Volkswagen la Ujerumani.

Hii ni mara ya pili kwa waziri huyo kufikishwa mahakamani na kuamuliwa akamatwe wiki iliyopita kwa ajili ya uchunguzi kuhusu kashfa ya ufisadi.

Wakati huohuo,  waziri wa zamani wa Fedha wa Algeria,  Karim Djoudi,  naye pia alifikishwa mahakamani  jana kujibu tuhuma za ufisadi.


Mahakama inachunguza kesi hizo za ufisadi huku maandamano ya wananchi bado yakiendelea nchini humo  baada ya Rais Abdelaziz  Bouteflika kujiuzulu ambapo wanataka wote wanaofungamana naye waondoke na waliohusika na ufisadi wakamatwe na wafikishwe kizimbani.


Loading...

Toa comment