The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Majaliwa Afurahishwa Na Mchango Wa Tigo Sekta Ya Madini, Kongamano La Madini Na Uwekezaji 2023

Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimsiliza kiumakini Mkuu wa Kitengo cha Masoko Huduma na TEHAMA Tigo Business Bwn. Norman Kiondo aliyekuwa akimpa maelekezo ya kazi wanazozifanya.

Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Leo Oktoba 26 ametembelea banda la Tigo katika Kongamano la Madini na Uwekezaji Tanzania (Tanzania Mining and Investment Forum 2023) lililohitimishwa jana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere ( JNICC)  Jijini Dar Es Salaam .

Waziri Mkuu Majaliwa amefurahi kufahamu kwamba kampuni hii imewezesha kongamano hili kwa namna kuu mbili, mosi,  kwa kutoa Intaneti ya BURE na yenye Kasi (FREE WI-FI) kwa washiriki wote wa kongamano hili kutoka ndani na nje ya nchi na Pili kama watoa huduma za mawasiliano kwa makampuni na mashirika mengi ambayo yapo katika sekta hii ya madini.

Akimwelezea Mhe. Majaliwa, Mkuu wa Kitengo cha Masoko Huduma na TEHAMA Tigo Business Bwn. Norman Kiondo amesema;

“Tigo kupitia masuluhisho yake mengi inaunga mkono agenda ya kitaifa ya kuiweka nchi katika dunia ya kidigitali na sisi kama kampuni tunayo masuluhisho ambayo yanasaidia makampuni yanayojishugulisha na madini kuweka kufanya shughuli zao katika namna ya kiteknolojia zaidi kuongeza ufanisi,  kupunguza gharama na kuongeza usalama wa wafanyakazi wao .”

Aidha Bwn.  Kiondo ameongezea kuwa  Tigo inayo masuluhisho kama Internet of Things (Iot) ambazo zimewezesha makampuni na mashirika mengi kuweza kufanya huduma zao kwa namna ya kiteknolojia huduma kama Ku TRACK Magari na vifaa vingine kuweza kujua vilipo na usalama wake kiujumla.  Huduma nyingine ni Kidigal Enabled Workforce ambapo mfanyakazi anapoingia sehemu kama mgodini anakua ameunganishwa na msimamizi wake anaweza kuona chochote kinachoendelea hii inaongeza ufanisi na usalama wa wafanyakazi.

Kwa upande mwingine,  wanafunzi kutoka Shule Kuu ya Madini na Jiosayansi Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam ambao ni Adelina Shilula,  Patrokil John,  Ambrose Leonard,  na Nassor Kimata wamefurahia mchango mkubwa wa Tigo katika sekta ya madini ambapo kila mmoja ameelezea furaha yake muda mchache baada ya kutembelea banda la Tigo katika kongamano hilo.