Waziri Mkuu Mstaafu wa China Li Keqiang Afariki Dunia kwa Mshtuko wa Moyo
Waziri mkuu wa zamani wa China Li Keqiang amefariki dunia kwa mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 68.
Alipotajwa kuwa kiongozi wa baadaye wa nchi hiyo, Li aliwekwa kando na Rais Xi Jinping ambaye, katika miaka ya hivi karibuni, amesisitiza kushikilia madaraka.
Vyombo vya habari vya serikali vilisema alikuwa “amepumzika” huko Shanghai alipopatwa na mshtuko wa moyo wa ghafla siku ya Alhamisi.
Aliaga dunia usiku wa manane siku ya Ijumaa licha ya “juhudi kubwa” za kumpatia matibabu, shirika la utangazaji la serikali CCTV lilisema.
Katika muhula wake wa mwisho akiwa waziri mkuu, uliomalizika mapema mwaka huu, Li alikua afisa mkuu pekee aliyeko madarakani ambaye hakuwa wa kundi la watiifu la Bw Xi.
Li, mtu wa pili mwenye nguvu katika Chama tawala cha Kikomunisti cha China hadi alipostaafu mwaka jana, alijulikana kama mmoja wa watu werevu zaidi wa kisiasa wa kizazi chake, akikubaliwa katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Peking mara baada ya vyuo vikuu kufunguliwa tena kufuatia maafa ya Mao, Mapinduzi ya Utamaduni.