Waziri Mkuu wa Latvia Atangaza Kujiuzulu Baada ya Kukosa Kuungwa Mkono
Waziri Mkuu wa Latvia, Krisjanis Karins leo Agosti 14, 2023 ametangaza kujiuzulu wadhifa wake pamoja na baraza lake la mawaziri.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Karins amesema amefikia uamuzi huo baada ya kukosa kuungwa mkono na vyama washirika vinavyounda serikali ya pamoja hivyo atawasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa rais wa nchi hiyo.
Miongoni mwa mambo yanayotajwa kuchangia uamuzi wake huo, ni kitendo cha vyama pinzani kupinga mabadiliko ya baraza la mawaziri aliyokuwa anataka kuyafanya.