The House of Favourite Newspapers
gunners X

Waziri Mkuu wa Uingereza Asifu Mwanzo Mpya Baada ya Brexit

0

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, ameusifu mwanzo mpya kwa Uingereza wakati ikijiandaa kuondoka Umoja wa Ulaya baada ya miaka 47.

 

Kiongozi huyo wa chama cha Conservative amesema ni wakati wa kuweka kikomo kwa miaka mingi ya mabishano makali kuhusu Brexit ambayo yameigawa nchi hiyo na kuongeza kuwa kazi yake kama serikali, ni kuiweka nchi pamoja na kuiendesha kwenda mbele.

 

Uingereza itaondoka katika Umoja wa Ulaya leo hii Ijumaa ya Januari 31 saa tano kamili usiku, ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu baada ya kupigwa kura ya maoni mwaka wa 2016 ya kujiondoa.

Leave A Reply