Video: Waziri Nape Amkabidhi Diamond Bendera Kuiwakilisha Tanzania Kwenye AFCON, Gabon

nape-nnauye-akimkabidhi-bendera-ya-kuiwakilisha-tanzania-abdul-diamod-1

DAR ES SALAAM: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye leo January 11, 2017 amemkabidhi nyota wa Afro Pop, Diamond Platnumz bendera ya Taifa ili kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye ufunguzi rasmi wa mashindano ya Africa Cup of Nation (AFCON) yanayotarajiwa kuanza nchini Garbon hivi karibuni.

nape-nnauye-akimkabidhi-bendera-ya-kuiwakilisha-tanzania-abdul-diamod-4Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauyeakizungumza jambo wakati wa hafla hiyo.

Hafla hiyo fupi ilifanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, imekuja ikiwa ni baada ya nyota huyo wa muziki kuteuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kwenda kutumbuiza kwenye uzinduzi wa mashindano hayo.

nape-nnauye-akimkabidhi-bendera-ya-kuiwakilisha-tanzania-abdul-diamod-2

Balozi wa DST ambaye ni komediani maarufu bongo, Lucas Mhuvile ‘Joti’ akizungumza jambo.

Nape amezungumza haya

“Siku ya leo nina furaha  kumuaga ndugu yetu Diamond na kundi lake amabapo wamepata fursa ya kuipeperusha bendera ya nchi yetu kwa dunia nzima.

“Kama nilivyosema kuwa AFCON ni mashindano makubwa na yanaangaliwa na dunia nzima kwa hiyo kwa tukio hili inaonyesha ni jinsi gani sanaa yetu ya Tanzania imekuwa kubwa ndio maana leo nipo hapa kwa niaaba ya Serikali kumpongeza Diamond na kumkabidhi bendera ya Tanzania.‘” alisema Nape.

nape-nnauye-akimkabidhi-bendera-ya-kuiwakilisha-tanzania-abdul-diamod-3

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  Multichoice Tanzania Salum Salum akizungumza jambo katika hafala hiyo.

“Diamond Platnumz alipokuja kuniambia alisema kuwa wanatarajia kwenda na timu kubwa Garbon hivyo tukajaribu kuwasaidia kidogo ndio maana mimi niliwafata Multchoice kupitia DSTV na wameweza kutusaidia tiketi sita za kwenda na kurudi kwa ajili ya msafara wa Diamond Platnumz‘” alieleza Nape.

Michuano ya AFCON 2017 inadhaminiwa na kampuni ya Total, na itaanza tarehe 14 January, 2017 na fainali itakuwa tarehe 05 Februari, 2017.

NA DENIS MTIMA/GPL

Waziri Nape Amkabidhi Diamond Bendera Kuiwakilisha Tanzania Kwenye AFCON, Gabon


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment