Waziri Nape na Mafanikio Aliyoyapata Kwenye Mwaka Mmoja wa Kuaminiwa
Mwaka Mmoja umepita tangu Rais Samia Suluhu Hassan, alipomteua Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Ndani ya kipindi hicho cha mwaka mmoja wa kuaminiwa, Waziri Nape amewezesha mambo mengi na ya muhimu kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa.
Miongoni mwa mambo hayo, ni pamoja na kukamilika kwa Programu Tumizi ya Mfumo wa Anwani za Makazi Nchini (NAPA), kufikishwa kwa huduma za mawasiliano Msomera na Tanzania kupata uanachama wa Baraza la ITU.
Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa uhuru wa vyombo vya habari, kuwezesha uchumi wa kidijitali na kupatikana kwa stempu ya pamoja kati ya Tanzania na Oman.