The House of Favourite Newspapers

Mwigulu amfukuza kazi mkuu wa mnada wa mifugo wa Pugu

0
Mwigulu (1)Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza na viongozi wa machinjio ya Vingunguti – Dar mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza usiku wa kuamkia leo.Mwigulu (2)…akipewa maelekezo
Mwigulu (3)…akikagua machinjio hayoMwigulu (4) Mwigulu (5)
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Lameck Nchemba, amemfukuza kazi mkuu wa mnada wa mifugo wa Pugu, na watumishi walioshiriki kuiba ushuru wa serikali, alipoenda machinjioni hapo kukagua.
Waziri Nchemba amesema alienda machinjioni hapo kutatua kero zinazowakabili wananchi na wadau wa machinjio hayo, huku akishirikisha wizara mbili ya Afya na TAMISEMI.
“Nimerejea asubuhi ya leo kwenye machinjio ya Vingunguti kwa ajili ya kutatua kero zinazowakabili watumiaji wa machinjio hayo, kutokana na uwepo wa ubadhilifu wa kodi ya serikali kwenye mnada wa pugu na malalamiko kadhaa yanayogusa wananchi wanaotumia machinjio haya, nimeshirikisha wizara mbili (TAMISEMI na AFYA) kutoa majawabu ya muda mfupi na ya kudumu”, alisema Waziri Nchemba
Baada ya kufika machinjioni hapo Waziri Mwigulu Nchemba alitoa maagizo kwamba Mkuu wa mnada wa machinjioni hapo watafute kazi nyingine, na kuwataka kufika ofisi ya Katibu Mkuu wa wizara.
“Nimeagiza kuwa Mkuu wa mnada wa Pugu na watumishi waliokuwa zamu tar. 24.12.2015 na tar.01.01.2016, kuanzia sasa watafute kazi nyigine, wakati huohuo wahakikishe wanafika ofisi ya Katibu mkuu wizarani kwangu mapema Jumatatu tar.04/01/2016”, alisema Waziri Nchemba.
Pamoja na hayo Waziri Nchemba amesitisha uchukuaji wa ushuru katika eneo la mnada wa Pugu, na kutaka makusanyo ya fedha zote yafanyike machinjio ya Vingunguti kwa kutumia mashine za EFD.
“Kuanzia sasa nimesitisha uchukuaji wa ushuru eneo la mnada wa Pugu, badala yake makusanyo yote ya fedha za serikali yatafanyika machinjio ya Vingunguti kwa kutumia mashine za elektroniki za EFD, kwa maana hiyo mnada wa Pugu utakuwa unatumika kutoa vibali tu vya mifugo ilikudhibiti ubora wa mifugo inayopaswa kuchinjw”, alisema Waziri Nchemba.
Pia waziri Nchemba ametaka eneo la kuhifadhia nyama lililokuwa limejengwa kwa fedha za wananchi kushirikiana na serikali lifunguliwe kwa ajili ya wananchi kulitumia kuhifadhia nyama.
Hatua za kuboresha miundombinu ya machinjio hayo zimeelekezwa kwa Halmashauri ya Ilala zifanyiwe kazi haraka na kwa ubora, na kutakiwa kurudishwa kwa umeme uliokuwa umekatwa eneo hilo, kwa ajili ya kuwarahisishia wananchi shughuli zao.

Leave A Reply