Waziri Ndejembi Atoa Ujumbe Mzito Kwa Watumishi Wasiokuwa Weledi – Video

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi saba wa wizara hiyo Mkoa wa Dar es Salaam kwa tuhuma za makosa waliyofanya kwenye sekta ya Ardhi.
Mhe. Ndejembi ametoa kauli hiyo mkoani Dar es Salaam wakati alipokutana na watumishi hao ambao wamekiri kuhusika na baadhi ya migogoro ya ardhi katika Mkoa huo ambapo kupitia kikao hicho Waziri wa Ardhi amemwelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuihusisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kushughulikia suala hilo.