Waziri Ndumbalo Atoa Maagizo kwa Rita Kuboresha Huduma Mikoani
WAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk Damas Ndumbaro ameilekeza Rita kuimarisha huduma zake katika Mikoa iliyo nje ya Dar es Salaam.
Waziri huyo ameilekeza Taasisi hiyo inayohusika na Usajili,Ufilisi na Udhamini nchini , kuhakikisha mikoani huko kunakuwa naa watumishi na vifaa vya kutosha ili kuweza kukabiliana na watu ambao sio waaminifu .
Ametoa maagizo hayo Jjini Dar es Salaam siku ya jana tarehe 10, Agosti,2022 katika hafla ya Kilele cha maadhimisho ya tano ya siku ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu Barani Afrika yaliyofanyika Shule ya Msingi Gongolamboto.
Katika Maadhimisho hayo yaliyofanyika shuleni hapo Waziri huyo alisema:
“Tanzania imeanza kuchukua hatua madhubuti ya kuongeza kasi ya usajili kupitia mkakati wa kitaifa wa usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu ambao tayari umeanza kutekelezwa kwa program mbalimbali lakini Rita kama chombo cha kutekeleza ni lazima mzingatie maagizo ili kuongeza weledi na kupata taarifa sahihi”
Dk Ndumbaro amesema Serikali bado inaendelea na kujipanga kuiboresha mifumo ya Tehama ili kuifanya Rita kuwa ya kidijitali kwa kuongeza matumizi ya technolojia katika usajili ili kuifadhi taarifa baadaa yaa kutambua taarifa kwa manufaa ya maendeleo ya Taifa.
Naye Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Slaa ameiomba taasisi hiyo kuweka nguvu katika kushughulikia tatizo la mirathi katika jamii.