Waziri Silaa Aingilia Mgogoro wa Ardhi Mapinga Uliotaka Zaidi ya Nyumba 100 Zivunjwe
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa ameingilia kati mgogoro wa ardhi uliozua taharuki katika eneo la Mapinga wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani kati ya wananchi zaidi ya 100 na mtu mmoja ambaye aliyejulikana kwa majina ya Sevestine Mtunga ambaye inadaiwa anamiliki eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 12 baada ya mahakama kuwataka wananchi hao kutakiwa kuondoka katika eneo hilo.
Mambo mawili ambayo hayana utata ni dhahiri Ntunga ameshinda shauri baraza la ardhi na ana haki, lakini pia ni dhahiri wananchi wako tayari kumlipa fidia na ni wito wake ni busara kukaa mezani na kumaliza kadhia hii tukizingatia msingi wa sera ya ardhi kwamba ardhi ni mali ya umma chini ya udhamini wa Rais.
Aidha Waziri Silaa ameelekeza zoezi hilo lisimame kwanza na kumuomba mwakilishi wa Sevestin Mtunga ampe muda ili serikali iweze kulifanyia kazi swala hilo ili kuondoa taharuki kwa wananchi kama maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kumwelekeza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash kukutana na pande zote kuanzia Jumanne Juni 18, 2024.