The House of Favourite Newspapers

Waziri Silaa Azindua Kampeni ya ‘Sitapeleki’ Kukabili Utapeli Mtandaoni

 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) akizungumza katika Mkutano wake na waandishi wa habari jijini Arusha Februari 21, 2025 kuitambulisha kampeni ya ‘Sitapeliki’ itakayofanywa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa pamoja na Makampuni ya simu nchini.

Pamoja na kuitambulisha kampeni hiyo mahsusi yenye lengo la kutoa elimu kwa umma ili kupunguza matukio ya watu kutapeliwa na kulaghaiwa mtandaoni, Waziri Silaa ametoa rai kwa watu maarufu na mashuhuri wenye wafuatiliaji wengi mtandaoni kushiriki kampeni hiyo kwa kuchapisha taarifa za kampeni hiyo kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii ili elimu hiyo iwafikie watanzania wengi zaidi.

Aidha, Waziri Silaa amesema watanzania wanalo jukumu la kujilinda na utapeli mtandaoni hasa namba za simu zilizosajiliwa kwa majina yao, namba za siri na simu yenyewe na iwapo wakikutana na matukio ya utapeli wanatakiwa kuripoti katika vituo vya polisi ili hatua ziweze kuchukuliwa na Wizara anayoiongoza kupitia TCRA itatoa ushirikiano kwa asilimia 100