The House of Favourite Newspapers

WAZIRI TIZEBA, MARSHA WAWASILI MSIBANI KWA SHIGONGO

Lawrence Marsha akisaini kwenye kitabu cha waombolezaji.

VIONGOZI mbalimbali wamejumuika na familia ya Eric Shigongo katika ibada ya mazishi ya mama yake, Bi. Asteria Kahabi Kapela,  ambaye atazikwa leo Agosti 1, 2018 nyumbani kwake katika kijiji cha Bupandwamhela kilichopo Buchosa, wilayani Sengerema.

 Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Yakobo Mkuu, Padri Hilary Faraja, Mwangika akiongoza ibada hiyo.

Baadhi yao ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba ambaye pia ni Mbunge wa Buchosa kupitia CCM, mbunge wa zamani wa Nyamagana na aliyekuwa waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Lawrence Marsha.

 

Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba akiwa kwenye ibada ya mazishi hayo.

Mbali namawaziri hao, wengine ni Mchungaji Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ na wengine.

Bi. Asteria Kapela alifariki dunia Ijumaa ya Julai 27, 2018 katika Taasisi ya Jakaya Kikwete Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

 

Masanja Mkandamizaji (wa pili kushoto mstari wa mbele) akiwa na waombolezaji wengine msibani hapo.

 

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho (katikati),  akielekea kuchukua nafasi yake kwa ajili ya kuanza ibada.

Comments are closed.