The House of Favourite Newspapers

Ummy Asema Hakuna Ebola Tanzania – Video

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amewatoa wasiwasi Watanzania juu ya uvumi wa kuwepo ugonjwa wa ebola hapa nchini ambapo amesema mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Septemba 14, 2019,  Ummy akiwa na naibu wake, Dk Faustine Ndugulile, Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Kambi,  na jopo la wataalam wa Shirika la Afya Duniani (WHO), amewataka wananchi kutokuwa na hofu yoyote.

Amebainisha kuwa taarifa za kuwepo kwa ugonjwa huo nchini zimetokana na watu wawili kudhaniwa kuwa na maambukizi ya ebola katika miji ya Mwanza na Dar es Salaam.

“Hawa walikuwa wahisiwa lakini wizara imefanya vipimo vya maabara zaidi ya mara moja kama inavyoelekezwa na mwongozo wa WHO na kujiridhisha kwamba hawakuwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo,  hivyo hakuna ugonjwa huo Tanzania,” amesema.

Comments are closed.