
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) akizungumza na mtoto wa marehemu Reginald Mengi, Abdiel Miku Mengi.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, leo Mei 4, 2019 amefika nyumbani kwa marehemu Dkt. Reginald Mengi, Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa ajili kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu.
Akizungumza wakati akitoa pole hizo, Ummy amesema kuwa kifo cha Dkt. Mengi ni pengo lisilozibika kwa kuwa alikuwa na msaada mkubwa katika sekta ya afya, na ameahidi kushirikiana na familia kufanikisha ujenzi wa kiwanda cha dawa kilichokuwa kimeanza kujengwa na Dkt. Mengi.
Mzee Mengi alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi Mei 2, 2019 nchini Dubai na mwili wake unatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu, saa 8:00 mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla ya kuagwa Karimjee, Posta, Jumanne, na kusafirishwa Jumatano kwenda nyumbani kwao Machame Kilimanjaro ambako utazikwa Alhamisi.


Comments are closed.