Waziri wa Fedha, Dk Mwingulu Ataja Takwimu za Kutisha Ajali Barabarani

Waziri wa Fedha, Dk Mwingulu Nchemba ameweka hadharani takwimu za kustaajabisha kuhusu ajali za vyombo vya moto 10,093 zilizosababisha vifo vya watu 7,639 na majeruhi 12,663.
Waziri Mwigulu amesema ajali hizo ambazo ni za kati ya mwaka 2019 na 2024 zinahusisha magari binafsi – ajali 3,250, vifo 2,090, na majeruhi 3,177.
Ajali za mabasi – 790, zilisababisha vifo 782, majeruhi 2,508. Ajali za daladala 820, zilisababisha vifo 777, na majeruhi 1,810. Wakati ajali za taxi – 93, zilisababisha vifo 97, na majeruhi 173.
Magari ya kukodi (sherehe, misiba, na shughuli maalum) yalipata ajali 326, na kusababisha vifo 263, na majeruhi 302.
Idadi hii haihusishi ajali za pikipiki, bajaj wala watembea kwa miguu.