The House of Favourite Newspapers
gunners X

Waziri wa Fedha na Mipango Awasilisha Ripoti ya CAG Bungeni

0

RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha wa 2021/22, imewasilishwa bungeni jijini Dodoma, kwa ajili ya kujadiliwa na mhimili huo.

Ripoti hiyo imewasilishwa bungeni leo Alhamisi, tarehe 6 Aprili 2023 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba.

Dk. Mwigulu amewasilisha ripoti ya ukaguzi wa CAG kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2022, pamoja na kaguzi nyingine.

Ripoti nyingine zilizowasilishwa na Waziri huyo wa fedha, ni ripoti ya mwaka ya ukaguzi wa CAG kwa Serikali Kuu kwa 2021/22. Ripoti ya CAG ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo, ripoti ya ukaguzi wa mashirika ya umma na ripoti ya jumla ya CAG ya ukaguzi wa ufanisi kwa mwaka huo wa fedha.

“Napenda kuwasilisha mezani taarifa ya ufanisi kuhusu utekelezaji wa maendeleo endelevu nchini, ukaguzi wa ufanisi kuhusu usimamizi wa uondoshaji magari ya Serikali na taarifa ya ufuatiliaji utekelezaji wa mapendekezo ya kaguzi za ufanisi zilizofanyika kwa kuwasilishwa bungeni Aprili 2018/19,” amesema Dk. Mwigulu.

Hatua hiyo inakuja siku kadhaa tangu baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Msukuma’ na Mbunge wa Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo, kuweka ahadi ya kuwanyoosha watumishi wa umma waliotajwa kuhusika na vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma, waliotajwa katika ripoti hiyo.

Wabunge hao katika nyakati tofauti, walimuomba Spika Dk. Tulia Ackson, atenge muda wa kutosha kwa ajili ya wabunge kuijadili ripoti hiyo ili kutafuta muarobaini wa vitendo vya ubadhirifu vinavyoibuliwa na CAG kila mwaka.

Spika Tulia aliwatuliza wabunge hao akiwataka wasubiri ripoti hiyo iwasilishwe bungeni kisha kupelekwa katika kamati za mhimili huo, baadae itawawekwa hadharani kwa ajili ya kujadiliwa.

Miongoni mwa maeneo yaliyotajwa katika ripoti ya CAG kuwa na dosari katika matumizi ya fedha za umma ni katika taasisi na mashirika ya Serikali, ambapo inadaiwa katika hati 900 zilizokaguliwa, hati 800 zinaridhisha, wakati 81 zikiwa na mashaka huku 10 zikiwa mbaya.

MVUTANO WAZUKA BUNGENI, MBUNGE KUCHAUKA na SPIKA TULIA KUHUSU BWAWA LA NYERERE – ”USITUTUME”…

Leave A Reply