Waziri Wa Mambo ya Ndani Amtaka RPC Kukomesha Kero ya Wizi Kikwajuni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, amemtaka Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi komesha kero ya wizi katika Shehia ya Kikwajuni Bondeni. Mhandisi Masauni ameyasema hayo mapema jana, Oktoba 28, 2024, wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu Jimboni, kwa Shehia za Mwembeni, Mwembeladu na Kikwajuni Bondeni iliyolenga kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi kwa utaratibu wa ‘Papo kwa Papo’.
