The House of Favourite Newspapers

Waziri wa Mambo ya Ndani Atimuliwa Kazi Kisa Maandamano ya Kuwatetea Waisrael

0

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amemfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani Suella Braverman, ambaye aliibua hasira kwa kuwashutumu polisi kwa kuwa wapole mno na waandamanaji wanaowatetea Wapalestina.

Serikali imetangaza leo Jumatatu, Novemba 13, 2023 kwamba Braverman ameondoka kwenye kazi yake kama sehemu ya mabadiliko ya baraza la mawaziri kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.

Baada ya kufukuzwa kwake, Braverman alinukuliwa akisema: “Imekuwa heshima kubwa katika maisha yangu kutumikia kama Waziri wa Mambo ya Ndani. Nitakuwa na mengi ya kusema baadaye.

Waziri Mkuu Sunak alikuwa kwenye shinikizo kubwa la kumfukuza Braverman, mwanachama mwenye msimamo mkali wa kulia, baada ya wakosoaji kumshutumu kuchochea mivutano katikati ya maandamano yenye utata ya wafuasi wanaopinga kitendo cha Israel kuishambulia Gaza.

Bado haijawekwa wazi mara moja ni nani atachukua nafasi ya Braverman, ambaye aliteuliwa kwenye wadhifa huo wakati Sunak alipokuwa waziri mkuu Oktoba 25, 2022.

Leave A Reply