The House of Favourite Newspapers

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Azindu Shule ya Kata ya Sekondari

0

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amezindu Shule ya Kata ya Sekondari Kihenzile iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.

Waziri Ulega amezindua shule hiyo anakusema kuwa ujenzi wa shule hiyo ya kata ni sehemu ya shule nyingi zilizojengwa nchi nzima na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Tunamshukuru Rais Samia kwa kutujengea shule hizi nchi nzima kwani zimesaidia kupunguza changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kutoka nyumbani kwenda shuleni,” amesema.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini ambaye pia Naibu Waziri Wa Uchukuzi David Kihenzile ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya miradi ambapo kwa mradi huo Serikali imetoa takiribani milioni 583 kwa madarasa na milion 100 kwa ajili ya nyumba mbili za Waalimu

Naibu Waziri Kihenzile amesema kukamilika kwa mradi kumetatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya wanafunzi ambapo walikuwa wakitembea umbali mrefu Kwenda na kurudi shule.

”NIMEKATA TAMAA MPAKA NATAKA NIUZE FIGO YANGU” – MAGE MIAKA 24 ALIYEJIKUTA ANAISHI KAMA KICHAA DAR

Leave A Reply