Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar Awataka Vijana Kuwa Wabunifu Kuendana na Sera za Uwekezaji
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Sharif Ali Sharif amewataka vijana wa Kitanzania kubuni miradi inayoendana na sera za uwekezaji katika nchi ili waweze kuwa sehemu ya kujenga uchumi wa nchi yao kwa vitendo.
Akizunguza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Watendaji wakuu Bora 100 wa mwaka
pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali zikiwemo kampuni zilizofanya vizuri mwaka 2024 Waziri Ali Sharif amesema vijana wana nafasi ya kufanya kampuni zao kutambulika katika soko la ndani na nje iwapo watatumia vyema mazingira mazuri ya uwekezaji ndani ya nchi yao.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Eastern Star Bw. Deogratius Kilawe ambaye ndie muandaaji wa tuzo hizo
kwa ushirikiano wa Kampuni ya The Global CEO Institute
amesema dhumuni la kuandaa Tuzo hizo ni kusherehekea uongozi bora, kukuza uvumbuzi, na kuhamasisha kizazi kijacho cha watendaji pia kukuza na kuweka viwango pamoja na kuleta mabadiliko chanya na matokeo ya kudumu katika tasnia na jumuiya tunazohudumia.
Bw. Kilawe ameongeza kuwa
ugawaji wa tuzo hizo umezingatia ubora wa kazi zilizofanywa na washiriki huku baadhi ya washindi wakisema tuzo hizo zinatia chachu kwa Kampuni za Kitanzania kuendelea kufanya vizuri mwaka hadi mwaka kwa kubuni bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko la Kimataifa.