The House of Favourite Newspapers

Waziri wa Saudia Arabia Amtaka Cristiano Ronaldo, Agusia Kuinunua Man United na Liverpool

0
Waziri wa Michezo wa Saudi Arabia Prince bdulaziz bin Turki Al-Faisal

WAZIRI wa Michezo wa Saudi Arabia Prince Abdulaziz bin Turki Al-Faisal amebainisha nia ya kutamani kumuona Cristiano Ronaldo akishiriki katika Ligi Kuu ya Nchi hiyo kufuatia kuvunjiwa mkataba wake na Klabu ya Manchester United.

 

“Nani ambaye hatamtaka Ronaldo kucheza kwenye Ligi yetu? Ni mfano wa kuigwa kwa vijana wengi sana duniani, yeye na Messi ningependa kuwaona wote kwenye Ligi yetu, wachezaji wakubwa. Hiyo itasaidia kuonesha namna gani Ligi yetu inakua na kipi tunakifanya katika kuhakikisha tunaleta maendeleo kwenye michezo.” alisema Prince Abdulaziz bin Turki Al-Faisal.

 

Katika hatua nyingine Waziri huyo amegusia uwezekano wa wawekezaji ndani ya nchi yake kuwekeza kwa kununua klabu za Manchester United pamoja na Liverpool ambazo kwa sasa zipo sokoni.

Nyota wa Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo

Amebainisha kuwa klabu za Manchester United pamoja na Liverpool zinaendelea kufanya vizuri kutokana na kuwa na mtaji mkubwa wa mashabiki na wanachama duniani kwahyo ikitokea kama wawekezaji wa Saudi Arabia wakapewa nafasi ya kununua vilabu hivyo basi itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza maendeleo ya soka nchini Saudi Arabia kwa kubadilishana uzoefu kwa mataifa hayo.

 

Amesisitiza kuwa hadi sasa Saudi Arabia inashirikiana vizuri na klabu ya Newcastle United ya nchini Uingereza ambayo inamilikiwa na Tajiri kutoka nchini Saudi Arabia

Leave A Reply