Waziri wa Ufaransa Asitisha ‘Kumbatiza’ Paka Wake

 

WAZIRI katika serikali ya Ufaransa,  Nathalie Loiseau,  amesitisha hatua ya ‘kumbatiza’ au kumpa paka wake jina la Brexit kama ilivyoripotiwa hapo awali siku ya Jumapili.

 

Ripoti hizo zilianza kuenea Jumapili kupitia gazeti Journal du Dimanche ambapo lilisema  zimetoka kwenye akaunti ya waziri huyo ya  Facebook.

 

Kwenye akaunti hiyo kulikuwa na maandishi yanayosomeka, “Mwisho nimeamua kumuita paka wangu Brexit”.

 

Ila ripoti kamili baada ya gazeti hilo kufanya mahojiano zilisema kwamba huo ulikuwa ni utani na waziri huyo hana paka kama ilivyodhaniwa hapo awali.


Loading...

Toa comment