The House of Favourite Newspapers

Waziri wa Ujenzi Zanzibar Azindua Dawati la Uwekezaji La Vertex

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Khalid Salum Mohamed amewapongeza Vertex International Securities kwa kuanzisha dawati la uwekezaji kupitia Shirika la Posta Tanzania.
Rai hiyo ameitoa hii leo katika hafla ya uzinduzi wa dawati hilo uliofanyika Serena Jijini hapa, akiamini ni hatua kubwa hasa kuona taasisi binafsi zikishirikiana na Serikali kufanya jambo jema na la kuigwa kama hilo.
Mohamed amesema, wananchi fedha wanazo akitolea mfano kule Zanzibar wavuvi wanapesa nyingi lakini shida ni kuziongoza pesa hizo ndio kazi kubwa ambayo inawakabili hivyo wakipewa elimu watabadilika.
Amesema mambo ya kifedha yanahitaji sana ubunifu hivyo anatarajia kuona matokeo chanya ambayo yatasaidia wananchi kujua vyema juu ya uwekezaji na kulitumia vyema dawati hilo.
Mkurugenzi mtendaji wa Vertex International Securities Mateja Mgeta amesema, huduma hiyo ni ushirikiano kati ya Vertrx na Shirika la Posta ikiwa na lengo ni kuboresha upatikanaji wa soko la mitaji nchini Tanzania, hata hivyo bado tunakabiliwa na pengo la ushiriki wa umma katika uwekezaji wa mitaji.Amesema sababu za Vertex kufanya kazi na Shirika la Posta ni kuweza kuwafikia haraka kwa kuwa Posta wana matawi zaidi ya 500 hapa nchini hivyo itakuwa vyepesi kuwafikia wengi nchini.
Amesema masoko ya mitaji yanajukumu muhimu ya kukusanya na kuendeleza ajira kwa watu wengi na pia kuchangia kikamilifu katika ujenzi wa Taifa.

Kwa upande wa Posta Masta Daniel Mbodo amesema wamejipanga kuhakikisha huduma hii inawafikia vyema wananchi na kufanya uwekezaji kupitia vituo mbalimbali ya Posta.