Waziri Wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Akagua Mradi wa Bagamoyo Sugar

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akiongozwa na HusseinSufiani (katikati) ambaye ni Mratibu wa Mradi wa Kimkakati wa kilimo cha Miwa na uzalishaji wa sukari unatekelezwa na kampuni ya Bagamoyo Sugar Limited katika kujionea shughuli mbalimbali wanazozifanya katika mradi huo.

 

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ametembelea mradi wa Kimkakati wa kilimo cha Miwa na uzalishaji wa sukari unatekelezwa na kampuni ya Bagamoyo Sugar Limited ili kukagua utekelezaji wa mradi huo.

Tumekuja kukagua maendeleo ya mradi huu kujua kama unachangamoto zozote tuweze kuzitatua alisema Dkt. Kijaji. Mradi huo ambao unatekelezwa kwa muda wa  miaka mitatu kwa sasa umefikia asilimia 95 ya utekelezaji wake.
Waziri kijaji amesema mradi huu ni moja ya Ushuhuda kuwa mpango Mkakati wa Taifa wa kuhakikisha Agenda ya Tanzania ya Viwanda vya kimkakati ili kutosheleza mahitaji ya bidhaa muhimu hapa nchini unafanikiwa kwa kushirikiana na Sekta binafsi.
Tunatarajia kurudi hapa tarehe tano mwezi wa saba kwani tumeahidiwa mradi  utakuwa umeanza uzalishaji kama walivyotuahidi.
Ajira za moja kwa moja.
Kampuni hii itakapokuwa imekamilisha uwekezaji wake tunatarajia kuwepo kwa jumla ya ajira za moja kwa moja zaidi ya 1500 za na zisizokuwa za moja kwa moja ni 3000.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akiwa katika eneo la mashamaba ya miwa huku akiongozwa na Hussein Sufiani ambaye ni Mratibu wa Mradi wa Kimkakati wa kilimo cha Miwa na uzalishaji wa sukari unatekelezwa na kampuni ya Bagamoyo Sugar Limited.

Thamani ya Mradi na manufaa Ya Mradi kwa Watanzania Kampuni hii inatarajia kuwekeza jumla ya Dola za Kimarekani zipatazo Milioni 193.75 ambazo zitawekezwa katika kilimo cha miwa, miundombinu ya umwagiliaji, ujenzi wa kiwanda, ununuzi wa mitambo, na vifaa mbalimbali vinavyohitajika..
Mahitaji ya Sukari na uzalishaji Mahitaji ni kati ya tani 550,000-600,000 kwa mwaka na inatarajiwa kupanda hadi kufikia tani 800,000. Kiasi kinachozalishwa kwa sasa ni takribani tani 300,000.
Mradi huu unatarajiwa kuzalisha tani 30000 utakapoanza na utakapokamilika phase zote tatu utazalisha tani laki moja (100,000) za sukari kwa mwaka.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mradi wa Kimkakati wa kilimo cha Miwa na uzalishaji wa sukari unatekelezwa na kampuni ya Bagamoyo Sugar Limited. Wengine katika picha ni baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC).

Serikali inafanya maboresho mbalimbali ili kuboresha mifumo  na kurahisisha utoaji wa huduma zote za vibali na usajiri kwa wawekezaji.
Lengo ni kuhakikisha kuwa tunakabiliana na changamoto zote za wawekezaji na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja kwa haraka ili wawekezaji waweze kuwekeza miradi yao waliokusudia katika kipindi husika bila kukwamishwa na huduma za Taasisi zetu.


705
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?




Toa comment