Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Komoro Akamatwa
Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Komoro na Kiongozi wa chama cha Orange, Daoudou Abdallah Mohamed, amewekwa kizuizini, Mwendesha Mashtaka wa umma, Daoudou Abdallah Mohamed akisema kuwa anatuhumiwa kwa kuhatarisha usalama wakala wa sheria, ghasia na utekaji nyara, propaganda na uchochezi na kuzua ghasia.
Siku chache kabla ya kukamatwa kwake, Kiongozi wa Chama cha Orange na Mgombea ambaye hakufanikiwa katika Uchaguzi uliopita wa Urais alidai kwenye mitandao ya kijamii kufuatwa na maafisa wa Polisi ambao walikuwa katika gari lisilokuwa na namba za usajili na kuwanyang’anya camera waliyokuwa nayo.
Mwendesha Mashtaka amesema Daoudou Abdallah Mohamed anadaiwa kuhatarisha wakala wa sheria katika kutekeleza majukumu yake, wizi na kunyang’anywa vitendea kazi.
Pia Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Ndani anashukiwa kufanya mikakati ya kuvuruga sherehe za kuapishwa kwa Rais Azali Assoumani lakini na kufanya propaganda za uasi, kuchochea ghasia na fujo.