The House of Favourite Newspapers

‘WEKEZA KWANGU’ WAANDAA HARAMBEE KUCHANGIA WALEMAVU

Katibu wa Wekeza Kwangu,Joseph Makuka, (katikati) akizungumza.
Makuka, (katikati) akiendelea kufafanua jambo.
Mwenyekiti wa Wekeza Kwangu,Marilyn Mbogo,(katikati) akizungumza jambo.
Picha ya pamoja.

 

 

Wanaharakati kutoka vyuo vikuu nchini, kupitia kampeni ya Wekeza Kwangu, wameandaa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wasichana walemavu kutimiza ndoto zao, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii kuepukana na unyanyapaa kwa walemavu.

 

 

Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari, wanaharakati hao wameeleza kwamba harambee hiyo, itafanyika April 27, 2019 katika kituo cha kuoshea magari cha Bay Wash kilichopo jirani na Rose Garden, Mikocheni  jijini Dar es Salaam ambapo wanaharakati hao wataosha magari ya watu mbalimbali, kisha fedha watakazolipwa zitatumika kuwasaidia wasichana walemavu.

 

 

“Tumeamua kuanza na kundi la wasichana wenye ulemavu kwa sababu hawa wanapata wakati mgumu zaidi kuliko hata wanaume wenye ulemavu. Wana mahitaji mengi ya msingi, kama taulo za kike, fimbo kwa ajili ya wasioona, vifaa vya kusaidia usikivu (hearing aid), mafuta ya kuzuia miale ya jua kwa wenye ulemavu wa ngozi na kadhalika.

 

 

“Mahitaji ni mengi lakini tutaanza na machache kutegemeana na mwamko tutakaoupata kutoka kwa Watanzania. Tunawaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi siku hiyo, lakini hata kwa walio mbali, wanaweza kuchangia kupitia akaunti yetu kupitia Benki ya CRDB, 015041659700 au kwa Tigopesa namba 0658 689 848,” alisema Marylin Mbogo, mwenyekiti wa wanaharakati hao.

 

 

Kwa upande wake, katibu wa wanaharakati hao, Joseph Makuka amesema watu mbalimbali mashuhuri wanatarajiwa kushiriki kwenye harambee hiyo wakiwemo wenyeviti wa taasisi mbalimbali za watu wenye ulemavu, na kuwaomba Watanzania wanaoguswa na changamoto zinazowagusa wasichana wenye ulemavu, wajitokeze kwa wingi.

 

Comments are closed.