WELLU AMKINGIA KIFUA STEVE

Wellu Sengo ‘Matilda’

MTU na chake! Mwigizaji mwenye umbo matata kunako Bongo Muvi, Wellu Sengo ‘Matilda’ ambaye amezaa na komediani Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amemkingia kifua mzazi mwenzake huyo kwa kusema haoni tatizo kwa mambo yake anayoyafanya mitandaoni hasa kuropoka juu ya ishu za mastaa wenzake.  Akizungumza na Gazeti la ijumaa, Wellu alisema hawezi kupitia kila anachokifanya Steve mitandaoni ila kama kuna kitu anaona kina tatizo, huwa anamshauri.

“Sioni sababu na siwezi kupitia kila kitu anachokifanya Steve mtandaoni. Unajua kila mtu ana hulka yake, labda na yeye ndivyo alivyo. Kwa hiyo mimi huwa naangalia vitu muhimu kama anakosea ndiyo tunakaa, tunashauriana,” alisema Wellu aliyezaa mtoto mmoja na Steve.

Stori: Neema Adrian, Dar


Loading...

Toa comment