The House of Favourite Newspapers

Wellu Awataka Watu Wamuache

0

MSANII wa filamu za Kibongo, Wellu Sengo ambaye ni mzazi mwenzake na muigizaji, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameeleza kuwa hajamtaja mzazi mwenzake kwenye posti yake aliyoandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, hivyo watu wamuache.

 

Akizungumza na Amani, Wellu alisema baada ya kuandika maneno kwenye ukurasa wake huo, watu wamekuwa wakisema kuwa amemwandikia baba mtoto wake huyo na inaonekana wamegombana lakini siyo kweli, bali alijisikia tu kuandika na siyo kwamba alimkusudia mtu.

 

“Nimeandika maneno hayo kwa sababu nimejisikia na wala sijataja jina la mtu kwa kuwa mimi na Steve tulishaachana, hakuna kinachoendelea kati yetu na sasa namlea mwanangu na ninahakikisha nampa kila anachostahili kupata kama mtoto,” alisema Wellu.

Stori: Neema Adrian

 

MAGONJWA MATANO YALIYOTIKISA DUNIA NA KUUA MAELFU YA WATU…

Leave A Reply