Wellu: Nitazaa mtoto mwingine na Nyerere

MSANII wa filamu za Kibongo, Wellu Sengo ambaye ali­zaa na mchekeshaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amedai kuwa anatarajia kuonge­za mtoto mwingine na mzazi mwenziye huyo.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Wellu alisema amefurahi kuwa mama na anap­enda sana watoto hivyo anategemea kuongeza mtoto mwingine na Steve Nyerere kwani ana malengo ya kuzaa watoto wanne.

 

“Kwa jinsi nnavyo­tamani na kupenda watoto nitaongeza mtoto mwingine soon na malengo yangu ni kupata watoto wanne hivyo namuomba Mungu anikamilishie malengo yangu,” alisema Wellu.

STORI: Imelda Mtema, Ijumaa Wikienda

Toa comment