The House of Favourite Newspapers

Wellu: Sina bifu na Steve

 

MSANII wa filamu Bongo,Wellu Sengo ambaye ni mzazi mwenzake na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameeleza kuwa licha ya kuachana na baba mtoto wake huyo hana bifu naye.

Akibonga na Za Motomoto News, Wellu alisema siyo lazima wapenzi au wazazi mkiachana mnakuwa na bifu kwani huo ni ushamba usiotakiwa na ukiendekezwa unaweza kumwathiri mtoto.

“Unajua kuna watu wengine wakiachana wanawekeana bifu, mimi siko hivyo kwa sababu tayari mimi na Steve tumezaa, kwa hiyo tukiwekeana bifu haitakuwa vizuri,” alisema Wellu.

Stori:NEEMA ADRIAN

Comments are closed.