The House of Favourite Newspapers

WELU AMFICHA MWANAYE KUHOFIA WAJA

Matrida Sengo ‘Welu

Sexy mama wa sinema za Kibongo, Matrida Sengo ‘Welu’, kwa mara ya kwanza amefunguka kisa cha kumficha mwanaye aliyezaa na msanii Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kwamba ni kutokana na kuhofia maneno ya waja (walimwengu).

Katika mahojiano maalum na Over Ze Weekend, Welu aliweka wazi kwamba, hapendi kuanika maisha yake mitandaoni kama wafanyavyo kwa kuwa yanapaswa kuwa siri ili awe na amani.

“Sikumuonesha mwanangu mitandaoni hadi alipofikisha mwaka mmoja, nilihofia maneno ya waja, lakini pia napenda kuwa kimya ili watu waone matokeo. Kuhusu ndoa siwezi kuzun-gumza chochote kwa sasa,” alifunguka Welu.

Comments are closed.