The House of Favourite Newspapers

Wema Afungukia Ukimya Wake, Atambulisha ‘Wema Sepetu Empire’ (Picha +Video)

Mwigizaji wa Bongo Movie na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu,  akifanya mahojiano na +255 Global Radio leo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

 

BAADA ya kuwa kimya kwa kipindi, muigizaji ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu,  amefika katika ofisi za   Global Group zilizoko  Sinza-Mori jijini Dar na kuanika sababu za ukimya wake huku akitambulisha kampuni yake mpya ya ‘Wema Sepetu Empire’.

 

Akizungumza mapema leo ndani ya +255 Global Radio, Wema aliyekuwa ameongozana na Director wake, Neema Ndepanya,  alisema kuwa ukimya wake ulikuwa ni sababu ya kujipanga kuja na tamthiliya kubwa ambayo itakuwa chini ya Wema Sepetu Empire.

Mahojiano yakiendelea.

“Wema Sepetu Empire ni kampuni ambayo ipo chini ya Endless Fame inayosimamia filamu zangu kwa muda mrefu. Siku zote naamini katika kula na wenzangu mimi siyo mchoyo hata marehemu Kanumba (Steven) aliniona na kunipa hii nafasi, kwa nini nisimpe mtu mwingine?  Mimi ni mwanadamu halafu ni mwanadamu mzuri, tatizo watu tu!

“Mtaani kuna wasanii wachanga wengi hawajui wanaanzia wapi wanaenda wapi? Nilikuwa napokea simu hata 200 hadi 300 kwa siku moja kutoka kwa hawa wasanii wachanga wakiniomba niwasaidie.

“Mimi pamoja na Neema tukasema tutakuwa na kikundi ambacho tutawaandaa na kuwakuza kisha tunawatumia katika kazi zangu.  Kama mliona kazi yangu ya Heaven Sent wengi wao siyo mastaa ni wasanii wachanga kutoka Wema Sepetu Empire,” alisema Wema.

 

Wema pia aliongelea kutojichanganya na wasanii wenzake wengi kutoka Bongo Muvi ambao wapo katika ‘movement’ ya SwahiliFlix.

“Siyo kwamba hawa wahusika hawakuniita au kuniambia chochote, wameniita lakini nimeshindwa kwa sababu mimi pia nina kitu kama hicho wanachotaka kukifanya. Nilikuwa nina Wema Sepetu APP nikaistopisha ili itengenezwe iwe kubwa sana mpaka Agosti.  Mwaka huu tutaizindua upya ambapo itauza kazi zangu zote na vitu vyangu vingi kuanzia filamu na tamthiliya zangu zote bila kusahau kipindi cha In My Shoes,” alisema Wema.

 

Tayari Wema Sepetu Empire imetoa ajira kwa wasanii wasiopungua 60 na kesho kuanzia saa 4:00 asubuhi katika Viwanja vya Leaders jijini Dar watafanya usaili wa kuwatafuta wasanii wengine zaidi ya 150.

Comments are closed.