Wema Aanzisha Darasa la Mapishi

MISS Tanzania mwaka 2006 na msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu amesema anaanza kutoa darasa la mapishi kwa kupitia App yake ya @wemaapp.

 

Akizungumza na Showbiz, mrembo huyo mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni alisema jinsi ambavyo watu wengi wamekuwa wakisifia chakula anachopika, ameona ni bora sasa akatumia nafasi hiyo kuingiza kipato.

 

“Hivyo nimeona bora niitumie hii nafasi kuanzisha darasa la mapishi ambalo litakuwa likiruka kwenye app yangu ya @wemaapp kila wiki, kwa hiyo wale mashabiki wangu wa dhati wakae mkao wa kula,” alisema Wema.

Mahakama Yamkatalia Kabendera Kumzika Mama Yake – Video

Toa comment