WEMA AELEZA ALIVYOPIGWA MILIONI 64

Wema Isaac Sepetu

 UKURASA mpya! Mwanadashosti kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ameeleza kuwa ameanza upya maisha kutokana na misukosuko aliokutana nayo ya kutapeliwa shilingi milioni 64 na aliyemdanganya anataka kumuoa, Patrick Christopher ‘PCK’. 

 

Akipiga stori na Gazeti la Ijumaa, Wema alisema kuwa mwanaume huyo alimtapeli kiasi hicho cha fedha hivyo amejifunza kutokana na makosa na anamuomba Mungu asirudie tena kosa kama hilo lililotokea maana angekuwa ameshafanya vitu vingi vya maana ambavyo vingemsaidia kwenye maisha yake.

 

“Nilipita kwenye kipindi kigumu sana jamani, nimerudi nyuma sana yaani kifupi naanza maisha upya na mpaka sasa siamini kile ambacho kilinitokea yaani kama mtu alinipumbaza sijui kwa nini ila kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa ndiyo kosa,” alisema Wema

Stori: Imelda Mtema, Dar


Loading...

Toa comment