The House of Favourite Newspapers

WEMA AFICHUA SIRI YA MAISHA YAKE

WEMA Isaac Sepetu ‘Madam’ amevunja ukimya, amefichua siri nyuma ya maisha yake, Ijumaa Wikienda linakudokeza.  Katika mahojiano maalum na Gazeti la Ijumaa Wikienda muda mfupi baada ya kuhojiwa na +255 Global Radio na kutambulisha ‘project’ yake mpya ya Wema Sepetu Empire, mrembo huyo alisema kuna siri kubwa juu ya maisha yake ambayo wengi hawaijui. “Watu wengi wanajiuliza, nimewezaje kuwa kwenye fame (umaarufu au ustaa) for all those years (kwa miaka yote hiyo 13) tangu nilipotwaa Taji la Miss Tanzania (2006).

“Yapo mambo mengi, lakini kubwa ni kutokata tamaa. Mimi nikisema ninataka kitu changu, lazima kifanikiwe, huwa sikati tamaa. Kila ninapoanguka huwa ninasimama kisha ninajifuta na kusonga mbele. “Najua mimi nina roho nzuri sana. Sijawahi kuua mtu, sijawahi kudhulumu mtu, nimeshasaidia watu wengi na wala sijawahi kusema vibaya. Kuanguka ni mambo ya kawaida tu kwani na mimi ni binadamu.

“Jambo lingine ni kwamba kile kidogo ninachopata huwa ninapenda kushea na wengine. Ndiyo maana hata kwenye hii project ya Wema Sepetu Empire nataka watu ambao hawajulikani ili wajulikane na kujipatia kipato. “Usisahau mimi ninapenda sana watu, ndiyo maana nao wananipenda. Kila kona nitakapopita nina watu wananipenda na mimi ninawapenda bila kujali ni watu wa aina gani. Watu wote mimi ni mashabiki wangu.

“Siri nyingine ni kwamba ninapenda sana ninachokifanya. Jamani napenda kazi yangu ya filamu, yaani ni Mungu tu anajua. Wewe niwekee mimi kamera mbele yangu uone, nafanya kwa furaha kwa sababu ninapenda ninachokifanya. “Nilijua kwamba ningeendelea kung’ang’ania kwenye urembo baada ya kutwaa taji nisingedumu muda mrefu.

“Ninamshukuru Kanumba (marehemu) kwa kuniona na kuniingiza kwenye filamu. Ni kitu ambacho nitadumu nacho hadi ninazeeka. Kwa hiyo wanaodhani nimekwisha watangoja sana kwani ustaa wangu nitadumu nao,” alisema Wema. Juzi Jumamosi Wema aliendelea na project yake hiyo mpya ambapo baada ya hapo ataanza kuzalishana mastaa wapya katika tasnia ya filamu za Kibongo.

Comments are closed.