Wema Afungukia Penzi na Mohombi

Wema Sepetu .

 

STAA mwenye nyota kali Bongo, Wema Sepetu amefungukia madai ya kubanjuka kimapenzi na mwanamuziki mwenye asili ya Congo, Mohombi Nzasi Moupondo na kusema kuwa ni shemeji yake na si vinginevyo.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi Wema alisema kuwa, watu waache kutabiri vitu bila kujua ukweli wenyewe, kwani alipiga picha na mwanamuziki huyo kama shemeji yake kwa rafiki yake.

Mohombi.

“Hivi kwa nini watu ni wepesi wa kuongea mambo? Mohombi ni shemeji yangu, kama watu wanataka kumjua mpenzi wangu watamjua hivi karibuni tu, kwani nimejipanga kumuanika ‘soon’ hivyo waache kuotea,” alisema Wema.

STORI: IMELDA MTEMA | RISASI JUMAMOSI

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment