The House of Favourite Newspapers

WEMA AIBUA JIPYA ISHU YA KUKONDEANA KWAKE ‘SIJAKATWA UTUMBO’

STAA mwenye nyota kali Bongo Muvi, Wema Sepetu ameibua jipya kuhusiana na ishu yake ya kukonda ambapo ameamua kufunguka kuwa, sababu hasa iliyomfanya awe hivyo ni msongo wa mawazo ‘stress’ na si kukatwa utumbo ili apungue kama watu wanavyodai.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Wema kwa mara ya kwanza aliweka ‘plain’ kuwa kipindi alichopitia kwenye lile sakata la kuvuja kwa picha zake za chumbani na Patric Christopher ‘PCK’ kilikuwa kigumu mno kwani alikuwa anapitisha hata siku tatu bila kula chochote mpaka anapepesuka.

 

“Watu nawashangaa sana, wanaona kukatwa utumbo ni kitu rahisi ee? Mimi nimekon­da kwa sababu ya mawazo makali niliyokuwa nayo na si vitu vingine maana nilikuwa kwenye wakati mgumu sana,” alisema Wema.

 

Akaongeza kwa kusema kwamba, licha ya kupungua anaufurahia muonekano wake mpya kwani kuwa mnene zaidi nayo siyo poa.

“Yaani hujui tu ninavyoufura­hia huu mwili wangu wa sasa, nimekuwa sio mzito tena na navaa nguo ambazo nataka na napendeza zaidi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, kwa kifupi najipenda hivi nilivyo,” alisema Wema.

STORI ZOTE: Imelda Mtema

Comments are closed.